Mshauri wa biashara Charles
Ranked #222 in Squidoo Community, #31,046 overall | Donates to Squidoo Charity Fund
Karibu kwenye blogu ya Mshauri wa Biashara Charles
Charles P.M.Nazi ni Mshauri wa biashara anayejishughulisha na kutoa ushauri wa biahshara kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa. Pia anatoa ushauri kwa wa uendeshaji wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGO. Ana uzoefu katika kazi ya ukaguzi na uendeshaji wa asasi za kifedha SACCOS kwa miaka 20. Ametunga kitabu cha biashara kiitwacho Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Ofisi yake iko Sinza Kwa Remi katika majengo ya Princess Agnes Nursery School.Kwa mawasiliano piga simu namba 255755394701 au tuma barua pepe cnazi2002@yahoo.com
PataKitabu cha mbinu za biashara kwa email
Napenda kuwaarifu kwamba kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri unaweza kukipata kwenye email yako kwa mfumo wa PDF. Kwa wale wanaohitaji wanaweza kunitumia Sh. 5000 kwa M PESA kwenye simu namba 0755394701 kisha kunitumia email zao na mimi nitawatumia email iliyoambatanishwa na kitabu.
CHARLES NAZI
Mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara
Maelezo mafupi kuhusu Kitabu cha Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri.
Kitabu hiki kinalenga kumsaidia mtu yeyote ambaye anatafuta utajiri kwa kufanya biashara ndogondogo hadi kubwa. Pia kinatoa maarifa, mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na umaskini, kinatoa elimu ya biashara na mbinu mbalimbali za namna ya kupata pesa kwa njia halali ili kukurahisishia safari yako ya kuelekea kwenye kutafuta na kupata utajiri. Kitabu hiki kina sehemu mbili, sehemu ya kwanza inaeleza kuhusu taratibu za kuanzisha biashara sheria, utafiti wa masoko, utunzaji wa hesabu za biashara na utatuzi wa matatizo ya biashara. Sehemu ya pili inaelezea kuhusu mawazo, mbinu mbalimbali za biashara unazoweza kuzifanya na kupata faida na hivyo kutajirika.
Mtunzi wa Kitabu hiki Charles P. M. Nazi ni mshauri wa masuala ya biashara.
Kitabu hiki ni matokeo ya utafiti na uzoefu ushauri na katika kazi za ukaguzi.
TzLinks

Blogu ya Mshauri wa biashara Charles
Malengo yake dira na mipango yake ya baadaye
MALENGO
Malengo yake ni kutoa huduma bora za ushauri kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa,kwa SACCOS na Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.
DIRA
Anaamini kwamba matatizo yanayozuia maendeleo ya Wajasiriamali Tanzania ni pamoja na ukosefu wa mitaji na elimu ya biashara,hivyo lengo lake ni kuhakikisha anatoa elimu ya biashara na uendeshaji ili biashara na asasi ziweze kuendeshwa kwa ufanisi.
MALENGO YAKE
1.Kutoa ushauri wa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa,
2.Kuandaa michanganuuo kwa ajili ya kuomba mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili..
3.Kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wafanyabiashara.
4.Kuandaa mifumo ya utunzaji wa mahesabu na kuweka mifumo ya Kompyuta kwenye utunzaji wa hesabu..
5.Kuandaa katiba za vyama na nyaraka za uandikishaji wa makampuni.
6.Kuandaa nyaraka za Tenda.
7.Kutoa ushauri kwa SACCOS ili ziendeshwe kwa ufanisi.
8.Kutoa ushauri kwa Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.
9.Kutunga vitabu za biashara ili kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi.
10.Kutoa ushauri nasaha na semina kwa wanafunzi.
MIPANGO YAKE YA BAADAYE
Kuimarisha biashara yake ili iweze kuenea mikoa yote ya Tanzania.
CHARLES P.M.NAZI
MSHAURI WA BIASHARA
free search engine submission
MAKALA YA LEO
Biashara ya kuku wa kienyeji inavyoweza kukuondolea umasikini.
Na Charles Nazi
Watu wengi wamekuwa wakifikiria kuhusu namna ya kujikwamua kutoka kwenye umasikini.Leo hii nitawaelezea kuhusu biashara ya kufuga kuku wa kienyeji ambavyo inaweza kukukwamua kutoka kwenye umasikini. Lengo kuu ni kuwawezesha watu kutengeneza ajira kwao binafsi na watu wengine.
Takwimu za uzalishaji (kutaga, kuangua na kukuza kuku)
Utafiti uliofanywa na Dr. John Bishop kwa msaada wa shirika la kitaifa la utafiti wa kilimo nchini Equador na Chuo kikuu cha Florida nchini Marekani, umeonyesha kuwa ; Kama kuku akitunzwa vizuri kutokana na mbinu bora za ufugaji, anaweza Kuongeza uwezo wa kutaga mayai kutoka mayai 10 hadi mayai 12 kwa mwezi. Kwa mfano ukiwa na kuku 12 na jogoo 1 waliolishwa kilo 1 ya nafaka kila siku unaweza kuuza dazani 10 za mayai kila mwezi ambayo ni sawa na mayai 4 kila siku.
Jee unapenda kutajirika kwa kufuga na kuuza kuku?
Angalia mchanganuo wa mahesabu mapato yako yatakuwa kama ifuatavyo, Kwa kipindi cha miaka 2. K wa mtaji wa Sh. 500,000/= kama una eneo la eka 1 na mabanda ya kutosha kiasi cha kuku 10,000. Ukianza kwa kufuga kuku 25 ( kuku 20 na jogoo 5) ambao utawanunua kwa Sh. 250,000.00. Hao kuku 20 wakianza kutaga vifaranga 10 kila mmoja wataangua vifaranga 200 watunze vizuri katika vifaranga hao tuchukulie majike yanaweza kuwa 150 ambao ndani ya miezi 6 au zaidi nao wataanza kutaga. Kipindi hicho utakuwa na kuku (200+ 25 =225.) Baada ya hiyo miezi 6 kuku watakaotaga ni 170 kila mmoja akipata vifaranga 10 mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku (1700+20+55=1775) ukiuza kuku 1,000 kwa bei ya Tshs. 10,000 utapata Tshs. 10,000,000/=. Mwaka wa 2 majike 775 yakiangua vifaranga 10 kila mmoja utakuwa na kuku 7,550 mwisho wa mwaka ukiuza kuku 3,000 kwa bei ya Tshs. 10,000 utapata Tshs. 30,000,000/= Hesabu hizi ni kwa makadirio ya chini sana kwani kama nilivyoelezea hapo juu kuku mmoja kama atatunzwa vizuri anaweza kuataga mayai kati ya 10 hadi 12 kwa mwezi.
.Kuku wa kienyeji wamekuwa wakifugwa kwa wingi vijijini kwa malengo ya kupata nyama na mayai kwa ajili ya familia husika na kwa ajili ya kupata pesa za kujikimu. Kuku na mayai ya kienyeji yana faida kubwa kiafya kutofautisha na kuku wakisasa ambao hukuzwa kwa kemikali. Idadiya kuku Tanzania inakadiriwa kuwa na jumla ya kuku Milioni 34 wanaofugwa na takribani 60.5% ya kaya zinazojishughulisha na kilimo. Hata hivyo uzalishaji wake umebaki kuwa duni kutokana na changamoto za wafugaji zifuatazo; Utunzaji duni , Udhibiti mdogo wa magonjwa, lishe duni, makazi duni, Uzaliano wa karibu, Teknolojia duni, Kukosekana kwa mtazamo/mwamko wa kibiashara.
Faida ya kufuga kuku wa kienyeji.
Ufugaji wa kuku wa kienyeji una manufaa mengi kwa mfano; Kuku hutumia eneo dogo kuliko wanyama wengine wa kufugwa, pia hutumia chakula kidogo hivyo ufugaji unaweza kuendeshwa bila kutumia mtaji mkubwa. Kuku wanaweza kupewa mabaki ya chakula pamoja na vyakula vya kujitafutia kama vile wadudu,mbegu na majani. Kazi za usimamizi wa kuku zinaweza kufanywa na mama na watoto. Kuku na mayai humpatia mfugaji chakula bora na kumuongezea mapato. Pia mfugaji ni kama mtu aliyewekeza fedha zake benki au kwenye kitegauchumi kingine ambapo kuku huweza kuongezeka kutokana na kuku kutaga na kuangua vifaranga kama faida inavoongezeka benki na kwenye vitegauchumi vingine. Mfugaji ni sawa na mtu aliyeweka akiba benki kwani akipata shida anaweza kuuza kuku na kulipa ada, mahari matibabu ya hospitali pamoja na shida zingine. Kuku wa kienyeji anasaidia kusafisha mazingira kwa kula wadudu na kuongeza rutuba kwa mbolea inayotokana na kinyesi cha kuku ambacho hakina kemikali. Mbolea hii ni nzuri sana na kama inazalishwa kwa wingi inaweza kuwa chanzo kingine cha mapato kwa mfugaji wa kuku. Kuna mjasiriamali ninayemjua anafuga kuku wengi anazo tani nyingi za mbolea hii na anauza mbolea ya mavi ya kuku kwa Sh. 600 kwa kiloba cha kilo 50. Kuku wa kienyeji ana uwezo mkubwa wa kuhimili magonjwa, hutaga mayai na kutunza vifaranga badala ya kutumia mashine. Kuku wa kienyeji anaweza kuishi nchi yoyote duniani bila kuathiriwa na hali ya hewa.
Aina za magonjwa ya kuku na jinsi ya kukinga magonjwa.
Wapatie chanjo kuku wako kwa afya bora. Wapatie kinga mara kwamara kila baada ya miezi 3. Magonjwa yafuatayo ndiyo huwa yanawashambulia kuku.
New castle
Dalili za ugonjwa huu ni kuku kushindwa kupumua, kukohoa na kutokwa na mate,kuwa na kinyesi cha rangi ya kijani, ugonjwa huu hauna dawa. Chanjo hutolewa machoni kwa njia ya matone.
Minyoo.
Dalili za mionyoo ni kuku kukosa hamu ya kula uzalishaji wa mayai kupungua. Ukiona dalili hizo waone wataalamu wa mifugo upate dawa.
Wadudu.
Utitiri husumbua kuku, kwa kuwasababisha kukosa usingizi,ngozi kuharibika,huathiri uzalishaji wa mayai. Ukiona dalili hizi wasiliana na wataalamu wa mifugo upate dawa.
Magonjwa ya mapafu.
Huathiri sehemu za kupitishia hewa na kuwa na sauti ya kukoroma. Hali hii hupunguza uzalishaji wa mayai na uzito wa kuku kupungua. Ukiona dalili hizi wasiliana na wataalamu wa mifugo upate dawa.
Mambo mengine unayopaswa kuyajua kama mfugaji wa kuku
Inapokuja katika ufugaji wa kuku wa kienyeji ,mbinu inayotumiwa kijijini ile kuku huachwa azurure katika boma bila uchungaji ama na uchungaji mdogo.Kuna matatizo mengi ambayo kuku hukutana nayo. Kuku halishwi vyema kwani hula masalio ya.chakula na mabaki mengine wanayoyapata. Vifaranga wadogo huachwa washindanie chakula na kuku wakubwa na huwa nyama rahisi kwa wanyama wanaowinda na kula nyama na husambaza magonjwa. Kuku hawapati maji ya kutosha na hawana mahali pa kujisetiri dhidi ya upepo na mvua ama kuwaweka salama dhidi ya wanyama wanaowinda na kula nyama bila kusahau wezi. kuku hutaga mayai ardhini na yanaweza kuharibiwa kwa urahisi na kuliwa na wanyama wengine. Sio kawaida kuku kupewa chanjo na matibabu dhidi ya magonjwa na vimelea. Matokeo ni kuku wengi huwa wagonjwa na hukua pole pole,hutaga mayai machache na nyama kidogo.
Ili kuhakikisha mapato mazuri kutoka kwa kuku wako,fanya yafuatayo:
Kuwapatia kuku mgao mzuri wa vyakula tofauti na maji safi.Kutemeana na kipindi cha mwaka,wataweza kujitafutia chakula kwa kukwaruza ardhi katika boma. Wapatie chakula cha ziada ili kuku waongeze uzani na kuku watage mayai mengi zaidi. Walishe vifaranga na chakula kilicho na protini kama mchwa ili wakue kwa haraka na wawe na afya. Wajengee kuku mahali penye giza na patulivu ambapo wanaweza kutaga mayai yao.Kuku huhitaji kujisikia wakiwa salama kutoka kwa wanyama wanaowinda na kula nyama na wapita njia. Kama kuku watasumbuliwa mara kwa mara watakuwa wakiviacha viota vyao na hii huathiri uanguaji wa mayai. Ikiwa nia yako ni utoaji wa mayai,ni vizuri kufuga kuku wa kike pekee.Jogoo mmoja anaweza kufugwa aangalie wanyama wanaowinda na kula nyama na kuwahudumia kuku.Wakati jogoo wa ziada wanapofikia umri wa kuuzwa,wanafaa kuuzwa,kuchinjwa ama kutolewa kama zawadi kuzuia jogoo kula chakula ambacho ni adimu na kupigana na kuwataabisha kuku. Ukubwa wa kundi unafaa kuafikiana na ukubwa wa nyumba au banda ,kiasi cha chakula unachoweza kununua na raslimali za chakula katika maeneo yanayokuzunguka. Usinunue kuku kutoka katika vyanzo ambavyo havijathibitiwa haswa vipindi milipuko ya magonjwa ni kawaida kwa sababu wanaweza kusambaza magonjwa kwa wengine. Toa chanjo mara kwa mara kulingana na ushauri wa watoaji chanjo na madaktari wa wanyama wa nyumbani. Vifaranga wachanga wanapaswa kuchanjwa dhidi ya magonjwa ya kawaida ya kuambukizana wakifika umri wa wiki 2-3.
Ikiwa kuku watataabika kutoka kwa ugonjwa sugu unapaswa:
1. Kuita daktari wa wanyama
2. Kumwtenga kutoka kwa wengine
3.Kuku anafaa kuuliwa mara moja kwa kutegemea jinsi ugonjwa ulivyo mzito na
anafaa kuchomwa ama kuzikwa katika kina kirefu ili kuzuia mbwa na wanyama wengine kuwachimba na kusambaza ugonjwa.
Angalia ni kuku wagani wana dalili za kutaka kuangua mara moja kwa mwezi na uwapatie matunzo ya ziada.
MBINU ZA BIASHARA 1
Na Charles Msuluzya Nazi
SIRI YA UTAJIRI
Watu wengi wanajiuliza, "Siri ya utajiri ni nini?" Jee ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa na ziada na faida. Kwa bahati mbaya sana, elimu hii haifundishwi darasani ila wanayo wafanyabiashara wachache na kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri na huendelea kuificha. Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza kuigundua siri ya utajiri. Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze kufanikiwa na wapate manufaa kwa kununua kitabu hiki nimeamua kuiweka siri hii wazi:-
- Siri ya kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi unaojipa, yaani unaoweza kuitoa ziada na faida.
- Siri ya pili ya kuelekea kwenye utajiri ni kujifunza na kujenga tabia ya kuweka akiba
- Siri ya tatu ni kuwekeza fedha hizo za akiba katika vitega uchumi ambavyo vinazalisha faida endelevu.
- Siri ya nne ni kujifunza namna ya kufanya biashara na kuanzisha biashara yako ili iwe indelevu.
Kuna njia mbili za namna ya kupata utajiri zenye uhakika. Njia ya kwanza ni njia ndefu ambapo wataalamu na watafiti wa masuala ya fedha wameigundua njia hii ni rahisi kuifuata kwa sababu haihitaji uwe na kipato kikubwa, wanashauri kwamba ujenge tabia ya kuweka akiba, anza kuweka akiba ya T.shs 1,000 kila siku sawasawa na TShs 30,000 kwa mwezi, matokeo yake ni kwamba kama utaweka akiba yako kwa kipindi cha miaka 65 bila riba yoyote utakuwa na akiba TSshs 23,725,000 (Milioni Ishirini na Tatu Mia Saba Ishirini na Tano Elfu). Kama utawekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa kila mwaka itazaa na kukuletea TShs 2,750,000,000 (Bilioni Mbili na Milioni Mia Saba Hamsini). Hesabu hii inaweza ikakutisha na usiamini macho yako lakini hiyo ni siri ya nguvu ya hesabu na riba kama alivyozielezea mwanafizikia Enstein kwamba katika dunia hii hakuna kitu chenye nguvu kama hesabu za riba. Pengine njia hii inaweza kuwa ni ndefu sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wetu hatuwezi kusubiri muda mrefu. Hivyo tungependa kuwa na mafanikio ya kiuchumi kwa haraka. Lakini nasisitiza kama kipato chako ni kidogo anza leo kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku.
Dundulizo la akiba hii hukutiririshia utajiri bila wewe kukusudia kwani utaweza kukidhi hitajiko la ghafla kama kuugua safari ya dharura gharama za likizo na hata kutumia mbinu hii kama mpango wa elimu kwa watoto wako iwapo utawaanzishia hivi mara tu kila mmojawapo anapozaliwa au unaweza kuutumia kama upanga wa siku zijazo kwa mirathi ukianza hivyo leo kwa kupangilia namna hiyo kwa kila kusudio lako la baadaye.
Hebu tuangalie njia ya pili.
- Njia ya pili ya mkato ni kuongeza kiwango cha kuweka akiba kama wewe ni mtu mwenye shughuli za kuzalisha ziada. Kipato chako kinaweza kuwa kinaongezeka kila mara. Badala ya kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku jiwekee malengo ya kuweka akiba ya TShs 10,000. Anza kwa kutenga asilimia 10% ya mapato yako hadi utakapofikia lengo la TShs 10,000 au zaidi kwa siku. Badala ya lengo lako kutimia kwa miaka sitini na tano (65) litatimia haraka zaidi. Kwa mfano ukiweka akiba ya TShs 10,000 kwa siku kwa muda wa miaka sita na miezi sita bila riba yoyote utapata TShs. 23,725,000. Ukiwekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa miaka sita na miezi sita utapata TShs. 33,917,505.78. Kama fedha hiyo utaendelea kuweka akiba kwa riba hiyohiyo hadi kufikia muda wa miaka kumi utapata TShs. 63,112,201.43.
Kwa kuwa kitu cha muhimu hapa ni kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo katika kitegauchumi chenye kutoa faida kubwa, utajiuliza jee uwekeze kwenye kitega uchumi chenye kutoa faida kiasi gani? Wataalamu wa mambo ya fedha wanashauri kuwa uwekeze fedha yako kwenye kitegauchumi chenye kutoa faida ya angalau asilimia 10% Kwa mfano unaweza kuwekeza kwenye Akaunti ya TAJIRIKA ya Standard Chatered Bank" inatoa riba ya asilimia kumi 10% pia unaweza kuwekeza kwa kununua hisa katika soko la hisa na mitaji.
Kwa wastani wa watafiti wa masuala ya fedha viwango vya mapato yatokanayo na hisa kwa gawio pamoja na kukua kwa mtaji ni zaidi ya asilimia 11% ambayo ni makubwa kwa kiwango cha kawaida cha asilimia kumi (10%).
Baada ya kueleza siri ya namna ya kupata utajiri nitazitaja njia zingine ambazo zinaweza kukuwezesha kuwa tajiri.
1. Unaweza kurithi mali na fedha kutoka kwa wazazi wako. Hii ni njia ya kubahatisha kwani watu matajiri siyo wengi na hivyo watoto wenye bahati kama hii ni wachache pia.
2. Unaweza kusomea ujuzi au utaalamu katika fani yenye malipo mazuri na kujiajiri mwenyewe. Kwa mfano, unaweza kusomea fani kama ya Uanasheria, Uhasibu na Udaktari au ufundi / sanaa na kadhalika.
3. Unaweza kuanzisha biashara yako na kuiendesha ili kupata ziada kubwa.
4. Unaweza kuendeleza vipaji vyako na kuwa mwanamichezo au msanii wa kulipwa.
5. Unaweza kutunga vitabu juu ya suala lolote unalolijua. Kwa mfano, kama wewe ni mtu uliyebobea katika masuala ya muziki unaweza kutunga kitabu kinachofundisha watu namna ya kuwa mwanamuziki. Watunzi wengi wa vitabu ni matajiri wakubwa. Hii ni kazi unayoweza kuifanya mara moja lakini ukavuna matunda yake kwa muda mrefu sana.
6. Unaweza kuwa mbunifu na kuanza kuuza mawazo yako au kutumia chombo ulichokibuni kukuingizia fedha.
7. Unaweza kucheza bahati nasibu na kushinda. Tatizo hapa soko na wateja wa aina hii ya huduma ni haba. Hiki ni kitu cha kubahatisha na nimekitaja makusudi ili kuwapa onyo wasomaji kwani watu wengi wanapenda sana kucheza michezo ya kubahatisha.
Uwezekano wa kutajirika kwa njia hii ni mdogo sana. Hivyo, nawashauri wasomaji kuachana na njia hii ya kutafuta utajiri. Nawashauri wachague njia yoyote inayofaa na inawezekana kwa kufuatana na mazingira yanayomzunguka mtu husika. Mkulima au mfugaji anaweza kuzingatia fani hii na kutajirika sana. Kwa kweli hakuna mipaka, hasa hapa kwetu Tanzania kwa sababu ya wingi wa fursa za kuweza kujishughulisha na kuwa tajiri.
Maelezo ya kina juu ya aina ya biashara au mbinu unaweza kuzitumia kutafuta na kupata faida utayapata katika sehemu ya pili ya kitabu hiki.
Inawezekana kuwa tofauti kati ya mtu tajiri na mtu maskini inatokana na kile tulichojifunza kutoka kwa wazazi wetu. Wazazi maskini huwaambia watoto wao wajitahidi kusoma sana ili wapate maksi nzuri darasani na ili baadaye waweze kupata kazi nzuri. Wakati wazazi matajiri huwapa watoto wao elimu ya namna ya kutafuta fedha. Kwa kawaida tukiwa shuleni tunapewa ripoti ya masomo. Katika maisha tunatakiwa kuwa na ripoti yetu ya maisha nayo ni orodha ya mali tulizonazo ikiwa ni pamoja na elimu ya kuzaliwa na ya kusomea na fedha taslimu zile zilizo katika hifadhi mbalimbali.
Kwa kufuata tafsiri ya Umoja wa mataifa mtu masikini ni yule ambaye kipato chake hakizidi TShs 1,000 kwa siku.
Inawezekana kuwa mfumo wa kifedha wa mtu maskini ni mfumo ambao humfanya kutumia kipato chake chote kulipia matumizi huwa hana ziada wala uwezo wa kuweka akiba hana madeni na hana mali.
Mfumo wa fedha wa mtu mwenye kipato cha kati ni mfumo ambao humfanya kuwa na mali kama magari, nyumba na kadhalika. Mara nyingi mali hizo huwa zinapatikana kwa mikopo na hutumia mshahara kulipia matumizi na madeni, hasa kama madeni ni makubwa, mtu mwenye kipato cha kati anapaswa kumuona mshauri wa maswala ya biashara. Hatua anazoweza kuchukua ili kujikwamua na tatizo la madeni anaweza kulazimika kuuza baadhi ya mali zake ambazo amezinunua kwa kutaka kuonyesha ufahari tu na ambazo hazina umuhimu. Kwa mfano kama mtu ana magari matatu ya kutembelea, anaweza kuuza magari mawili kubaki na gari limoja na fedha atakayoiokoa kuiwekeza au kutumia kama mataji na kuanzisha biashara ili kujiongezea kipato.
Mfumo wa mtu tajiri ni mfumo ambao unamwezesha kuwa na biashara yake, kumiliki mali nyingi, kuwa na fedha nyingi katika akiba na awe ameziwekeza kwenye vitega uchumi vinavyolipa faida kubwa zaidi ya asiliamia kumi, kama vile nyumba za kupangisha na hisa. Mtu huyu hana wasiwasi na maisha. Anaweza kusafiri au kuugua lakini vitegauchumi vyake vinaendelea kumwingizia fedha. Siri kubwa ya matajiri ni uwezo wa kutumia fedha na kuziwekeza kupata faida kubwa.
Hiki ni kitabu cha vitendo. Yote unayoyasoma humu inabidi uyafanyie kazi ili yakusaidie. Tofauti kati ya maskini na tajiri iko katika kuchukua hatua. Tajiri hujifunza mambo ya kumwendeleza na kuchukua hatua kwa kutekeleza kwa vitendo yale anayojifunza na anayoyaona yanaweza kumuinua kiuchumi. Maskini huwa anajifunza mambo na kuyaacha kichwani bila kuchukua hatua au kuyafanyia kazi aliyojifunza na hivyo fursa ya kupata utajiri inampita hivihivi. Kwa hiyo, kama unataka kuwa tajiri anza mara moja kufanya yafuatayo:-
1. Anza kuweka akiba ya T.Shs 1,000 kila siku. Tengeneza kisanduku na tumbukiza TShs. 1,000 kila siku. Zikifika TShs. 50,000 kafungue akaunti ya TAJIRIKA, kwenye Benki ya "Standard Chatered". Kisha endelea kuweka TShs. 30,000 kila mwezi. Jinsi mapato yako yatakavyokuwa yanaongezeka tenga asilimia kumi (10%) ya mapato yako uweke akiba kila mwezi. Lengo lako liwe ni kuweka TShs 10,000 au zaidi kila mwezi. Fedha unayoweka ni kama unapanda mbegu. Kumbuka hii ndiyo hatua ya kwanza kuelekea kwenye utajiri. Faida katika benki hii ni kubwa. Inaanzia asilimia 6.5% kwa kianzio cha TShs. 50,000 hadi TShs. 5,000,000 na asilimia 10% kwa kiwango kinachozidi TShs. 10,000,000. Fedha utakazoziweka huko usiziguse mpaka ukiona zimekuwa nyingi ndipo utaamua na kupanga ukaziwekeze sehemu gani.
2. Jifunze pia mbinu za kutafuta fedha. Njia rahisi ni ya uhakika ya kukuwezesha kufanikiwa kiuchumi katika maisha ni kutafuta mshauri au mtaalamu anayejua mbinu za uongozi wa biashara ili akushauri vizuri juu ya yale unayonuia kutekeleza.
3. Inawezekana pia bado hujawa na biashara ya aina yoyote. Kama ndivyo anza kufanya utafiti kuona utafanya biashara gani. Mawazo ya biashara gani ufanye unaweza kuyapata katika sehemu ya pili ya kitabu hiki. Kila mara hakikisha unatenga asilimia 10% ya mapato yako na kuweka kwenye akaunti yako ya TAJIRIKA. Kumbuka kwamba kuwa na biashara yako ni siri ya pili ya kuelekea kwenye kupata utajiri. Kama unayo biashara yako unaweza kumtafuta mtaalamu wa biashara kuangalia jinsi unavyoweza kuiboresha au kuipanua.
4. Panga malengo ya muda wa mwaka mmoja miaka mitano na miaka ishirini ili kuhakikisha kwamba unajikomboa kiuchumi. Malengo yako makuu yawe ni:- kuwa na akiba ya fedha za kutosha katika akaunti yako , kuwa na biashara yako, na vitega uchumi vya aina tofauti ambavyo unaweza kuvisimamia vizuri.
5. Kama wewe ni mwajiriwa, kipimo chako cha mafanikio kiwe ni kujiuliza swali, kama utaacha kazi yako ya mshahara utaweza kuishi kwa kutumia kipato chako cha pembeni kwenye biashara yako kwa muda gani? Mafanikio yako yatakuja pale utakapoweza kutumia kipato chako cha ziada bila kutegemea mshahara, na hapo ndipo unaweza kuacha kazi na kwenda kuimarisha biashara zako au kuendelea na kazi huku pia ukijiimarisha kibiashara.
6. Kama utafuata mpango wa namna hii na kujituma kwa juhudi na maarifa kwa muda wa miaka mitano (5) unaweza kuwa tajiri na maisha yako yanaweza kuwa mazuri.
CHARLES MSULUZYA NAZI
Mwandishi wa makala hii ni mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Kwa mawasiliano piga simu namba 0755394701 barua pepe cnazi2002@yahoo.com au tembelea tovuti yake www.mshauriwabiashara.com
MBINU ZA BIASHARA 2
Na Charles Msuluzya Nazi
NAMNA YA KUANZISHA BIASHARA.
Ukitaka kufanya biashara yoyote ile unatakiwa kufanya utafiti. Kutokufanya utafiti ni chanzo cha biashara nyingi kuharibika. Lazima ujiulize kwamba unataka kufanya biashara gani? Usiseme unataka kufanya biashara yoyote ile kwani kusema kwamba unataka kufanya biashara yoyote ile ni kupoteza mwelekeo kwa kuwa utakuwa hujui unataka kufanya nini. Kama hujui cha kufanya hakuna kitu utakachokifanya. Hili ni tatizo la watu wengi. Hata baadhi ya watu niliokutana nao wakitaka ushauri wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili. Njia ya kukusaidia kuamua ufanye biashara gani ni kwa kujiuliza umewahi kufanya kazi au biashara gani? Umesomea nini? Vipaji vyako ni vipi? Ni biashara ipi au kazi ipi unapenda zaidi kuliko nyingine na kwa sababu gani? Ukisha jiuliza maswali haya chukua kalamu na karatasi uandike maswali yako na kuyajibu. Ukikagua maswali na majibu yako utagundua shughuli unayoipenda, unayoiweza na una kipaji nayo na hiyo ndiyo inayokufaa. Ukishachagua biashara unayoipenda ni rahisi sana kufanikiwa kwani shughuli utazifanya kwa hiyari bila kujilazimisha. Kama unashindwa kuamua ni biashara gani ufanye, soma sura ya sita katika kitabu hiki. Nimeelezea kuhusu mawazo yanayoweza kukusaidia kuanzisha biashara mbalimbali ambazo unaweza kuzifanya. Kama utakuwa bado hujafikia uamuzi baada ya hapo basi tafuta na wasiliana na washauri ili mbadilishane mawazo na ufundishwe jinsi ya kuamua ufanye biashara gani.
Mambo mengine unayotakiwa kuyafanyia utafiti ni:-
(i) Kujua siri ya bishara unayotaka kufanya ili upate mbinu za kupata mafanikio. Unaweza kupata siri au kujifunza mbinu kutoka kwa watu wanaofanya biashara kama unayotaka kufanya. Suala hili ni gumu sana kwani wafanyabiashara wengi huwa wanaficha siri za biashara zao ili kulinda wasizidiwe maarifa na washindani wao. Unaweza kuipata siri hiyo kama utakwenda kupata ushauri toka kwa mfanyabiashara ambaye yuko mbali na mahali unapofanyia biashara, au tafuta ushauri kwa wataalamu wa mambo ya biashara.
(ii) Fanya utafiti wa soko la bidhaa unazouza au unazotarajia kuuza. Jiulize, je bidhaa unazotaka kuziuza zina soko? Utawauzia watu gani na utauzaje? Kama wewe ni mzalishaji, una mazao / bidhaa unapaswa kuuza kwa jumla, mchanganyiko ama rejareja? Je utatangaza vipi bidhaa zako? Maelezo ya namna ya kutangaza bidhaa zako utayapata katika Sehemu ya Tatu ya Kitabu hiki. Utafiti wa soko unaweza kuufanya kwa kuwauliza wafanya biashara waliotangulia maswali hayo ya utafiti kwani wao wamekuwapo kwenye soko na wanazijua siri za soko.
(iii) Tengeneza bajeti yako kwa kuorodhesha vitu vinavyohitajika na gharama zake ili kuweza kuanzisha biashara yako. Vitu hivyo ni:-
(a) Gharama za Kujenga au kupanga ofisi
(b) Gharama za Leseni ya biashara
(c) Makadirio ya kodi toka TRA
(d) Garama ya vifaa vya ofisi yaani, Samani, makaratasi, mitambo, mashine, nk
(e) Manunuzi ya malighafi au bidhaa za kuanzia biashara
(f) Idadi ya wafanyakazi na gharama za mishahara yao.
(g) Gharama nyinginezo kama vile, umeme, maji, nk.
(iv) Unatakiwa kujua ni mtaji kiasi gani unahitajika kuanzisha biashara yako. Mtaji huo utaujua baada ya kujumlisha gharama zilizoorodheshwa katika kupengele namba (iii)Gharama hizi ni za mwaka ule wa kwanza wa kuanzia
(v) Tafuta Mtaji.
Mtaji unaweza kupatikana kutoka kwenye vyanzo vifuatavyo:-
(a) Akiba au mshahara
(b) Msaada au mkopo kutoka kwa ndugu na jamaa.
(c) Kuingia ubia na mtu mwenye mtaji
(d) Mkopo toka baadhi ya asasi kama vyama vya akiba na mikopo (SACCOS), NGO za kifedha sipokuwa Benki kwani hizi huwa hazitoi mikopo kwa mtu anayeanzisha biashara.
TARATIBU ZA KISHERIA ZA KUFUATA ILI KUANZISHA BIASHARA
Baada ya kufanya utafiti na kupanga mipango ya kuanzisha biashara unatakiwa kwanza kuangalia taratibu za kisheria ambazo unatakiwa kuzifuata na kuzitekeleza. Kama biashara yako ni ndogo anza kama mtu binafsi. Faida ya kuanza biashara kama mtu binafsi ni urahisi wa kuanzisha biashara; urahisi na wepesi wa kutoa maamuzi kwani huhitaji ridhaa ya mtu mwingine kabla ya kutoa uamuzi; mtaji unaohitajika utakuwa mdogo kutokana na gharama za uendeshaji kuwa ndogo, biashara hii inaweza kuendeshwa kwa msaada wa familia kwa kumtumia mke au mume, watoto au ndugu na jamaa na raslimali za familia kama nyumba na samani. Unapoanzisha biashara na kuiendesha mwenyewe unakuwa huru tofauti na mifumo mingine. Matatizo ya kufanya biashara kama mtu binafsi ni:- Kushindwa kupanua biashara yako kwa ufinyu wa mtaji; kufilisiwa mali zako za binafsi iwapo biashara yako itafilisika kwani katika mfumo huu mali ya biashara na mali binafsi si rahisi kuzitenganisha; Kuongeza mtaji inakuwa ni vigumu, hivyo unaweza kushindwa kupanua biashara yako. Ili kuepukana na matatizo niliyoyataja hapo juu unaweza kuungana na watu wengine kufanya biashara kwa ubia. Faida za kufanya biashara kwa ubia ni: Kupata fursa ya kuongeza mtaji kwa kushirikiana na wafanyabiashara wengine ambao wataleta mitaji yao; Kuongeza ujuzi katika shughuli kwa kuleta wataalamu pale taaluma Fulani inapohitajika. Matatizo ya kuendesha biashara kwa njia ya ubia ni: Kufilisiwa mali zako binafsi endapo biashara yako itafilisika; kudhulumiana mali endapo moja wa wabia atakuwa si mwaminifu ambapo anaweza kuingia mikataba mibovu na kusababisha hasara ambayo itabebwa na wabia wote. Ni muhimu kuwachunguza watu tunaotaka kujiunga nao ili tujue kama ni waaminifu. Pia ni vyema kuwapo na mkataba wa maandishi mnapoanzisha biashara ya ubia mkimshirikisha mwanasheria kama shahidi ili kujikinga na kudhulumiana; Kufariki kwa mbia mmoja kunaweza kusababisha kuvunjika kwa ubia; kotokuelewana kwa wabia kunaweza kusababisha kuvunjika kwa ubia. Kama biashara ikikua unaweza kuanzisha kampuni. Mfumo wa uendeshaji wa kampuni unazo faida zifuatazo: unatenganisha majukumu ya wamiliki mali na kampuni yaani kampuni inaposajiliwa inakuwa inakuwa na hadhi na kutambulika kisheria kama ni mfumo tofauti na wamiliki. Mfumo huu unatenganisha majukumu kati ya menejimenti na wamiliki wa kampuni; madeni ya kampuni yatalipwa hadi kufikia kikomo cha mtaji uliowekezwa na wamiliki. Hivyo, mali binafsi za wamiliki wa kampuni haziwezi kukamatwa kufidia madeni ya kampuni endapo kampuni itafilisika. Mfumo wa kampuni unatoa nafasi ya kupanua mtaji kwa kukusanya mitaji kwa kuongeza wanahisa au kupitia soko la mitaji ya hisa. Mfumo huu ndiyo unafaa kwa biashara kubwa kwani unatoa nafasi ya kupanuka kwa biashara na kuendelea kuwapo kwa biashara hata kama baadhi ya wamiliki wake wakifa au kujitoa katika kampuni.
Mambo ya muhimu ya kutekeleza kisheria kabla ya kuanzisha biashara ni:-
(a) Kuwa na ofisi
(b) Kukata leseni
(c) Kusajiliwa na TRA kama mlipokodi na kupewa namba ya mlipakodi
(d) Kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato ya awali
(e) Kutimiza masharti mengine ya keshiria kuwa mfano kama wewe unataka kufanya biashara ya ukandarasi wa ujenzi wa majengo lazima usajiliwe kwenye Bodi ya Wakandarasi.
Kama unafanya biashara ya kati au kubwa unapaswa kufuata sheria. Ni makosa kufanya biashara bila kufuata sheria za nchi. Hata hivyo, kuna biashara zingine ndogo ndogo sana kiasi kwamba uanzishaji wake si rahisi kufuata sheria hizo hapo juu, mfano uuzaji wa maandazi, karanga na vitu vingine vidogovidogo. Hizi zinaitwa biashara zisizo rasmi au biashara ndogondogo. Ni vyema ukachunguza kama biashara unayoifanya ni ndogo au kubwa ili ujue kama unapaswa kufuata taratibu za kisheria au la, kwani kutokujua utaratibu na sheria siyo kinga ya kukufanya usishitakiwe.

Mfahamu mwandishi wako wa makala za ujasiriamali
Watu wengi wamekuwa wasomaji wa makala zangu kwa muda mrefu bila kunifahamu, na wengine wamekuwa wakinipongeza kwa kazi nzuri ya makala nilizoandika. Kwa leo ningependa niwaeleze mimi ni nani ili mnifahamu vizuri. Mimi naitwa Charles Paul Msuluzya Nazi ambaye ni mwandishi wa makala za ujasiriamali katika gazeti la Mtanzania kila siku ya jumanne. Nilizaliwa mwaka 1958 huko Mbogwe Wilaya ya Bukombe na nilisoma Shule ya Msingi Mbogwe na baadaye Sekondari Ihungo mwaka 1975 hadi 1978 ambapo baada ya kumaliza kidato cha nne nilijiunga na Chuo cha Ushirika na maendeleo ya jamii Tengeru. Baada ya kumaliza mafunzo niliajiriwa na serikali nikiwa ni Afisa Ushirika msaidizi wilaya ya Mahenge mwaka 1981 hadi 1983 ambapo nilijiunga na Shirika la Masoko Kariakoo nikiwa ni Mkaguzi wa mahesabu ya ndani. Mnamo Mwaka 1988 nilijiunga na Shirika la Umeme TANESCO nikiwa ni Mkaguzi Mwandamizi wa mahesabu ya ndani, ambako ndipo nilipo hadi sasa. Mbali na kufanya kazi za za Mwajiri wangu nimekuwa pia nikijishughulisha na kazi zangu binafsi pamoja na kuhudumia jamii. Miongoni mwa kazi nilizozifanya ni Kuongoza Soko kuu SACCOS nikishika nafasi ya Katibu na Mweka hazina kuanzia mwaka 1985 hadi 1988. Katibu wa TANESCO SACCOS toka 1997 hadi mwaka 2005. Pia mnamo mwaka 2005 na 2010 nilishiriki katika kura za maoni kuomba kugombea Ubunge wilaya ya Bukombe na jimbo la Mbogwe kupitia CCM ambapo sikupata kura za kutosha kuteuliwa kugombea ubunge. Mimi nimeoa na katika familia yetu tumebahatika kupata watoto 5 wa kike 3 na wa kiume 2.
Kuhusu shughuli zangu binafsi Mimi ni mjasiriamali ambaye nimefanya shughuli mbali mbali na kubuni miradi mbali mbali, kwa mfano nimewahi kuanzisha kampuni ya Ujenzi, kiwanda kidogo cha chaki, kuendesha biashara ya mtandao kupitia Makampuni mbali mbali ya kigeni , biashara hizi nimeachana nazo. Sasa hivi najishughulisha na kutoa huduma ya Ushauri wa biashara. Huduma ambazo nazitoa ni; Kutoa ushauri wa biashara kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa, Kuandaa michanganuuo kwa ajili ya kuomba mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili, Kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wafanyabiashara, Kuandaa mifumo ya utunzaji wa mahesabu na kuweka mifumo ya Kompyuta kwenye utunzaji wa hesabu, Kuandaa katiba za vyama na nyaraka za uandikishaji wa makampuni, Kuandaa nyaraka za Tenda, Kutoa ushauri kwa SACCOS ili ziendeshwe kwa ufanisi, Kutoa ushauri kwa Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, Kutoa ushauri nasaha na semina kwa wanafunzi.
Mimi ni mtunzi wa vitabu na nimetunga kitabu cha Ujasiriamali kinachopendwa sana, kiitwacho, Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Kitabu hiki nilikitunga baada ya lengo la kuwafikia wajasiriamali kwa nja ya semina kukwama ambapo nilikuwa nikitoa matangazo kwenye magazeti lakini watu hawafiki. Kitabu hicho kinalenga kumsaidia mtu yeyote ambaye anatafuta utajiri kwa kufanya biashara ndogondogo hadi kubwa. Pia kinatoa maarifa, mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na umaskini, kinatoa elimu ya biashara na mbinu mbalimbali za namna ya kupata pesa kwa njia halali ili kukurahisishia safari yako ya kuelekea kwenye kutafuta na kupata utajiri. Kitabu hicho kina sehemu mbili, sehemu ya kwanza inaeleza kuhusu taratibu za kuanzisha biashara, sheria, utafiti wa masoko, utunzaji wa hesabu za biashara na utatuzi wa matatizo ya biashara. Sehemu ya pili inaelezea kuhusu mawazo na mbinu mbalimbali za biashara unazoweza kuzifanya na kupata faida na hivyo kutajirika.
Kitabu hicho ni matokeo ya utafiti na uzoefu katika kazi za ukaguzi nilizozifanya kwa kuangalia matatizo ya uendeshaji wa biashara mbalimbali pamoja na ushauri nilioutoa kwa watu walioomba ushauri kutoka kwangu. Kitabu hicho kilichapishwa kwa mara ya kwanza na Business Printers mwezi March mwaka 2008 na mpaka sasa zimechapishwa nakala 4,000 na kuuza nakala 3,000 kwa muda wa miaka 3.Kitabu hicho kiapatikana kwa njia ya Posta au email katika mfumo wa PDF unaweza kunitumia Sh. 5000 kwa MPESA Kwenye simu namba 0755394701 kisha ukanitumia email yako nami nitakutumia kwenye email yako kama kiambatanisho.
Mafanikio yangu ni pamoja na kupata wateja wengi waliopata ushauri wangu na kuufurahia. Pia niliweza kupata wateja wengi walionunua kitabu changu na kukifurahia. Baada ya kuchapisha kitabu nimehojiwa na vyombo mbali mbali vya habari kama vile; ITV, Star TV, TBC 1 TV na TBC1 Radio na Wapo Radio. Hata hivyo kila palipo na mafanikio hapakosi matatizo. Nimekuwa na malengo ya kuwa na kipindi changu cha Ujasiriamali ambacho kimekubalika na vyombo vya habari mbalimbali pamoja na wasikilizaji na watazamaji, lakini nimekosa wadhamimini wa kukidhamini kipindi hiki ambacho kinapendwa sana na wajasiriamali.
Malengo yangu ya baadaye ni kuhakikisha kwamba elimu ya ujasiriamali inaenezwa nchini Tanzania. Pia kuendelea kutoa huduma bora za ushauri kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa,kwa SACCOS na Asasi zisizo za kiserikali NGO ili ziweze kuendesha shughuli zao kwa ufanisi. Ili kutekeleza hayo nitafanya yafuatayo; Kutoa elimu kwa njia ya makala, Radio, Televisheni na semina na Video ya ujasiriamali. Ninao mpango wa kutunga vitabu zaidi katika masuala ya Ujasiriamali saikolojia na ushauri nasaha. Mimi ni mwana harakati wa kupigana vita na umasikini ambaye pia naamini kwamba umasikini hapa Tanzania utatoweka pale ambapo elimu ya ujasiriamali itakapokuwa imeenezwa kila sehemu, kwani watu wengi wanakosa fursa za kiuchumi au kujiingiza katika uwekezaji mbovu kwa kukosa maarifa. Pia naamini katika kutenda. Tatizo la Watanzania wengi ni kuwa na tabia ya kulalamika na kulaumu pale wanapokutana na mtatizo, lakini hawajitumi na wala hawatafuti maarifa na njia za kutatua matatizo.
Nawashauri viongozi wa Serikali pamoja na wadau wengine waweke utaratibu wa kufundisha elimu ya jasiriamali kwa vijana wetu kuanzia Shule za msingi hadi elimu ya juu ili mara wamalizapo shule wawe waajiri kwa kuwa wajasiriamali badala ya kuwa waajiriwa. Pia nashauri Serikali kutilia mkazo elimu ya juu kwa watanzania ili kuwakomboa Watanzania. Nchi zilizokazania elimu kwa watu wake, kama vile India, Japan na China, wamejikuta wakiwainua watu wake ambao walipata ajira nje ya nchi na kuinua uchumi wan chi kwa ujumla. Eneo lingine ambalo ninaloliona kuwa linatakiwa kuangaliwa ni uwezeshaji wa wananchi kwa kupatiwa mitaji. Utaratibu unaoweza kutumika ni kutoa ruzuku si kutoa mikopo kwa wajasiriamali kwani wengi hawana uwezo au ujuzi wa kuizungusha mikopo hiyo na kurejesha. Mbinu nyingine inayoweza kusaidia kuwainua wananchi ni njia ya kuanzisha asasi za wananchi zitakazo wafundisha utaratibu wa kujiwekea akiba na kukopeshana mfano VIKOBA pamoja na SACCOS. Ninaishauri Serikali kuweka mkazo kwenye kilimo hasa cha Mashamba makubwa na kuanzisha viwanda vya kusindika mazao kuyaongezea thamani badala ya kuuza kama malighafi ambapo bei yake ni ndogo. Pia serikali iangalie kuweka utaratibu mzuri wa masoko ya mazao ya wakulima hasa wadogo wadogo ili kuondoa umasikini wa kipato kwani tatizo lao kubwa ni masoko ya kuuzia mazao yao. Wataalamu wa uchumi wameonyesha kwamba nchi zote zilizoweka mkazo kuwekeza katika kilimo uchumi wake uliinuka haraka sana na huwa hauyumbi yumbi.
Ninatoa ushauri kwa wajasiriamali kwamba wakitaka kuanzisha biashara wasikurupuke wafanye utafiti kwanza kuhusu masoko na siri za biashara wanayotaka kuifanya.Wanaweza kufanya utafiti kwa kuwauliza watu waliofanikiwa katika biashara hizo au washauri wa biashara kama mwandishi wa makala za ujasiriamali na mshauri wa biashara. Kwa kuwa tatizo la watu wengi ni mtaji waanze kujenga tabia ya kujiwekea akiba kidogo kidogo na kufanya biashara ambazo zinaanza na mtaji kidogo halafu wapanue biashara kidogo kidogo. Mfano wa biashara ambayo wanaweza kuanza kwa mtaji kidogo ni ya Ufugaji wa kuku wa kienyeji na bustani. Kama wewe ni mjasiriamali mwerevu, ili ufanikiwe unapaswa kutafuta ushauri kutoka kwa wataalamu kwa ajili ya kutatua matatizo yako.
CHARLES NAZI
Mwandishi wa makala hii ni Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri,. Kwa ushauri wa biashara na kuandaliwa michanganuo kwa ajili ya mikopo na misaada tuma barua pepe, cnazi2002@yahoo.com piga simu namba 0755394701 au tembelea tovuti hii;
http://www.mshauriwabiashara.com

Great Stuff on Amazon
Vitabu ambavyo vimebadilisha nmaisha yangu
Angalia vitabu ambavyo vimebadilisha maisha yangu unaweza kuvipata katika maduka mbali mbali ya vitabu.
Video za ujasiriamali
Video za ujasiriamali jinsi kuhusu mbinu za biashara
video ya mbinu za biashara ya Bwana Charles Nazi
curated content from YouTube
New Del.icio.us bookmarks
Sorry, we couldn't connect to Del.icio.us. Please try again later.
New Amazon Voting (Plexo)
Unakipenda kitabu kipi?
Kama unakipenda kitabu chochote hapa waambie na wenzako
Rich Dad Poor Dad: What the Rich Teach Their Kids About Money-That the Poor and the Middle Class Do Not! by Robert T. Kiyosaki
Personal finance author and lecturer Robert T. Kiy more...0 points
Rich Dad, Poor Dad for Teens: The Secrets About Money--that You Don't Learn in School! (Miniature Edition) by Robert T. Kiyosaki
Following the highly successful Rich Dad Poor Dad, more...0 points
Padre Rico, Padre Pobre/ Rich Dad, Poor Dad (Padre Rico Advisors) (Spanish Edition) by Robert T. Kiyosaki and Sharon L. Lechter
A #1 New York Times bestseller, Rich Dad, Poor Dad more...0 points
Rich Dad's Guide to Investing: What the Rich Invest in, That the Poor and the Middle Class Do Not! by Robert T. Kiyosaki, Sharon L. Lechter
Rich Dad's Guide to Investing is a guide to unders more...0 points
Blog Posts from Google
Tafuta blogu
blogu maarufu za kiswahili
Link List
Pata mitandao maarufu ufaidike bure
Ifuatayo hapa chini ni mitandao maarufu ambayo unaweza kuitembelea na kufaidika bure
- Kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri
- Pata kitabu cha mbinu za biashara ambacho kinaweza kukusaidia kupambana na umasikini kwa njia halali
- Jiunge na mtandao wangu wa marafiki Tanzania upate taarifa mbali mbali
- Pata marafiki kupitia mtandao wa marafikitz ulimwenguni kote
- Tembelea mtandao maarufu Tanzania ambao una zaidi ya wanachama 30,000
- mtandao unaoongoza kwa kuwa na wanachama wengi na unatembelewa na watu wengi kila siku Tanzania
- Ping your blog free
- Ping your blog here it is free
- How to publish and sell ebook for free
- Learn how to publish a book free
- Marafiki Tanzania
- Blog ya marafiki Tanzania pata marafiki dunia nzima tembelea blog hii
- Internet marketing tips lens
- A blog which teaches how to market online
- Mshauri wa biashara
- Tovuti ya Charles P.M.Nazi Mshauri wa biashara anayejishughulisha na kutoa ushauri wa biashara kwa Wafanyabiashara wadogo wa kati na wakubwa. Pia anatoa ushauri kwa wa uendeshaji wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGO. Ana uzoefu katika kazi ya ukaguzi na uendeshaji wa asasi za kifedha SACCOS kwa miaka 20. Ametunga kitabu cha biashara kiitwacho Mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Ofisi yake iko Sinza Kwa Remi katika majengo ya Princess Agnes Nursery School.Kwa mawasiliano piga simu namba 255755394701 au tuma barua pepe cnazi2002@yahoo.com
- How to become a milionaine with 1000 ideas
- Blog that teaches you how to become a millionaire
- Mshauri wa saikolojia Charles
- Blog ya mshauri wa saikolojia Charles
- Charles Business cosultants Lens
- Charles Business consultant Blog dealing with providing business consultancy services to SMEs in TANZANIA
- Charles Nazi Official personal lens
- The official blog of Mr Charles Nazi
- How to make money online
- Free money making ideas and tips
Twitter Follow
Nifuate kwenye twiter
nifuate kwenye twiter
Google Blog Search
Pata habari na makala zangu
angalia makala zangu na habari zingine
Flickr Photos
Milion dolars
milion dolars
by cnazi2002
Hello world. This is my bio. I can edit it later! Charles P.M.Nazi is a Business Consultant and internet marketer he also deals with providing Business... more »
- 9 featured lenses
- Winner of 4 trophies!
- Top lens » Mshauri wa biashara Charles
Feeling creative?
Create a Lens!